WANAWAKE wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi wa jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini Spain. Mafunzo na mradi huo vinafadhiliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa  inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu waSpain Mama  María Teresa Fernández de laVega.

Taasisi hiyo itafanya kazi na wanawake hao 15 wa kitanzania kupitia miradi inayosaidia nchi kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Wanawake hao ambao kati yao watano ni waandishi wa habari kila mmoja atatekeleza mradi mmoja, huku waandishi wa habari wakisaidia kupaza sauti za akinamama hao kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Mradi huu unaojulikana kama GREEN VOICES una lengo la kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo unaoratibiwa hapa nchini na Mtandao wa wanahabari wa Mazingira (EMNet) kwa niaba ya Foundation for Women of Africa unatekelezwa katika mikoa sita ya Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani ukihusisha miradi ya kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.

Mratibu wa EMNet Secelela Balisidya amesema akinamama hao wanatekeleza miradi ambayo inachangia moja kwa moja aidha kupambana au kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema miradi hiyo ni mradi wa kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani na ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro. 
Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na viongozi wa Foundation For Women of Africa na wafadhili wa mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa mradi huo Madrid, Spain hivi karibuni.
Mama Maria Tereza (katikati) - Rais wa taasisi ya Foundation for Women of Africa akiwa na waandishi wa habari wanaotekelza mradi wa Green Voices wakati wa hafla ya kuwakaribisha kinamama nchini Spain. Kutoka kushoto ni Secelela Balisidya, Tukuswiga Mwaisumbe, Farida Hamis, Siddy Mgumia na aliyechuchumaa Judica Losai.
Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo kikuu cha Universitad Automous De Madrid, mara baada ya kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid, Spain hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...