Na JacquilineMrisho - MAELEZO

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyokuwa ikipinga kuondolewa kwa shitaka la 8 la utakatishaji fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake wawili. 
Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Moses Mzuna alipokuwa akitoa majibu ya rufaa iliyokuwa imekatwa na DPP. 
“Ninafahamu kila kesi inaamuliwa kutokana na mazingira yake lakini nimefuta rufaa hii kwa kuwa hoja zilizotolewa hazina nguvu kisheria” alisema Jaji Mzuna. 
Aidha Jaji Mzuna amefafanua kuwa hata kama amefuta rufaa hiyo lakini upande wa Jamuhuri bado una nafasi ya kubadilisha shitaka au hati nzima ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao. 
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Timony Vitalis amekubaliana na uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu ya pingamizi lake ingawa bado anasimamia watuhumiwa kutofutiwa shitaka la utakatishaji wa fedha. 
Naye Wakili wa Utetezi Majula Magafu amesema kuwa wao wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na Wakili wa Serikali ili wajue namna ya kuikabili kesi hiyo.
 Watuhumiwa hao; aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (wa mwisho kulia haonekani pichani), Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania Shose Sinare wakipeana mikono na Mawakili wao,ndugu jamaa na marafiki mahakamani hapo mapema leo mara baada ya Mahakama kuu leo Mei 06 2016 Kusikiliza rufaa ya kufutiwa shitaka lao namba nane la utakatishaji fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...