Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dokta Agnes Kijazi ameshukuru AZAM TV kuwa kituo cha kwanza cha Habari hapa nchini kuchukua jukumu la kushirikiana na mamlaka hiyo ili kutimiza viwango vya mamlaka ya hali ya hewa duniani katika kutangaza taarifa za hali ya hewa. Dokta Kijazi ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya wiki tatu ya kutangaza Taarifa za hali ya hewa kwa watangazaji wapya wa habari ya hali ya hewa ambazo huandaliwa na mamlaka ya hali ya hewa nchini.
Mafunzo ya hali ya hewa kwa jamii kwa wanahabari wa Azam yamefanyika kwa kuandaliwa na TMA na WMO, lengo ni kuimarisha uhusiano kati ya mtoa huduma na jamii kupitia vyombo vya habari.
Wanahabari wa Azam walipata wasaa wa kujifunza namna ya kurekodi na kutangaza utabiri wa hali ya hewa ili kuweza kuboresha vipindi vyao vya kwa jamii hususan kipindi cha habari.katika picha hapo wakatikati mbele ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Dokta Agnes Kijazi.

Pichani kutoka kulia ni mkuu wa chuo cha hali ya hewa Kigoma Joseph Aliba, Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dokta Agnes Kijazi, Samuel Muchemi (mwakilishi kutoka mamlaka ya hali ya hewa Duniani),   Mwanga Kirahi Mkurugenzi wa mafunzo Azam TV nyuma yao ni watangazaji wapya wa habari za hali ya hewa. Kutoka kushoto ni Mohamed Mohamed, Jamaly Hashim, Fatuma Mohamed, Sophia Kilumanga, Halima Shebuge, Rajabu Mbogo na Nuru Mbura.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...