Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi ya kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani  (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) kwa mara ya kwanza umeshiriki kwenye matembezi ya kusherehekea siku ya Wafanyakazi, maarufu kama MAY DAY jijini Dar es Salaam leo Mei 1, 2016.

Matembezi hayo yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka sekta ya Umma na Binafsi, ambazo ndio wadau wakubwa wa Mfuko huo, yalianzia kwenye ofisi za Shirikisho la Vyamavya Wafanyakazi, TUCTA, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kupita barabara ya Nkurumah, Nyerere na kisha kupinda barabara ya Chang’ombe hadi uwanja wa Uhuru ambako yalipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.

WCF ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.

Tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo, juhudi za kutangaza hudumazake kwa wadau zimekuwa zikiendelea mfululizokwa kutoa elimu kupitia semina, maonyeshona makongamano lakini pia kupitia vyombo vyahabari na kwa siku ya Mei Day imekuwa ni fursa kubwa ya WCF kuungana na wadau wake wakubwa.
 Wafanyakazi wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya kilele chasiku ya wafanyakazi Duniani
 Matembezi yakiwa yameingia Uwanja wa Uhuru.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...