Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Jacob Boniface akizungumza, wakati akitoa taarifa ya kusimamishwa kazi kwa Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Richard Chidaga.

Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/4/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bw. Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza Mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.

Kufuatia makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, Baraza la Madiwani la tarehe 4/05/2016, limeamua kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Richard Chidaga.

Makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo ni: 

1. Miradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa, Manispaa ilipaswa kupata shilingi Milioni 900 kwa mwaka kwa uwekezaji huo. Lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba Mapato hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi Bilioni 4.5 mpaka sasa. 

2. Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota, Manispaa  iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota, hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa Nyumba hizo longer, wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika Nyumba na kutoa madai ya kujengewa nyumba ama kulipwa fedha za fidia kutokana na Usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama liamuru Manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji nje ya mahakama. 

Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja. Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo kwa mchanganuo wa shilingi 695,520,000/= pango la mwaka na 2,576,000,000/= fidia ya viwanja 644.

3.Uwekezaji eneo la Coco Beach Oysterbay, Manispaa iliingia mkataba na Q - Consult Limited, Kampuni hiyo ilishindwa kutekelezwa mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-Consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini haikuwa na hatua zozote zilizochukuliwa na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na Serikali Mwanasheria Mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa Mwanasheria alikuwa hajakata rufaa. 

4.Mradi wa Ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital Ltd) Mkataba juu ya uendeshaji wa stendi haina manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1% ya makusanyo kwa mwaka sawa na Shilingi Milioni 4 tu kwa mwaka, wakati kabla ya uwekezaji, local standy Halmashauri ilikuwa ikipata Milioni 12 kwa mwezi.

5. Kubomolewa kwa ofisi ya Kata ya Msasani, mwananchi ajulikanaye kwa jina la Chacha aliingilia eneo la ofisi ya kata ya Msasani na baadae kuishtaki Manispaa. Usimamizi dhaifu wa shauri hilo kuisababishia mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaendeleaje. Hata hivyo kwa makusudi Bw. Chacha aliamua kuuza Kiwanda hili kwa Lake Oil CO. Limited wakati shauri halijaisha.Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo, yangu upande wa pili ulikataa Jaji, tuna zaidi ya mwaka hatujapangiwa Jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.

6. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment) Hill Road Oysterbay, mradi inafanyika kwa ubia na mwekezaji Texas Enterprise Company Ltd, mkataba uliingiwa mwaka 2009, na mradi umesimama kwa muda mrefu sasa.Pamefanyika mabadiliko katika mkataba na mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital. 

7. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment s) Kiwanda no. 314 Toure Drive.
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited mkataba uliingiwa 2009.

Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila idhini ya Halmashauri na kuisababishia mradi kuchelewa kukamilika, Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi.

Halmashauri bado inaendelea kufuatilia miradi mwingine ambayo umeingia na haina manufaa kwa Halmashauri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...