Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SIKU  chache baada ya pazia  la ligi kuu ya soka Tanzania  bara kufungwa, Kocha mkuu wa Mbeya  City Fc, Kinnah Phiri ameanza zoezi maalumu la kusaka nyota wapya ambao atawajumuisha  moja kwa moja kwenye vikosi vya timu yake  msimu ujao.

Akizungumza baada ya majaribio ya siku ya kwanza  kwa wachezaji wapya vijana waliofika kujaribu bahati zao kwa kuonyesha  vipaji walivyonavyo navyo, Afisa habari wa City Dismas Ten amesema kuwa muitikio umekuwa mzuri katika siku hii kwanza ambayo nyota hao wa baadae wamefika kuonysha  uwezo wao mbele ya kocha huyo raia wa malawi.

“Leo ni siku ya kwanza, kitu kizuri mwitikio umekuwa mkubwa, takribani vijana 50 wamejitokeza kujaribu  bahati zao kulingana na vipaji walivyonavyo, haya ni majaribio ambayo kocha Phiri ameyaitisha ili kusaka vipaji vipya ambavyo moja kwa moja vitaingia kwenye timu yetu kubwa na ile ya U20,"amesema Ten.

Kwa upande wa vijana waliojitokeza wameshukuru kuwepo kwa zoezi hili kwa sababu limerahisisha  uwezekano wa vipaji walivyonavyo kuonekana mapema hatimaye waweze kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji wakubwa  siku za usoni

Hii ni kawaida ya timu hiyo kila inapomaliza msimu wa ligi kuweza kuandaa programu inayowapa fursa vijana kuonyesha vipaji vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...