Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Halfan Mshiro pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema wakiokota baadhi ya uchafu katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta walipozuru kaburi hilo katika kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi na kulia ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
Mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi (watatu kulia) akiongoza dua ya kumuombea baba yake hayati sheikh Kaluta Amri Abeid wakati ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kushoto mbele) akizungumza wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni maoni yangu tu asikwazike yeyote. Nadhani inapendeza zaidi na ndivyo itakiwavyo kiimani, khususan kwa wanawake kujistiri vile itakiwaivyo inapotokea ziara ya kwenda kuzuru makaburi na khasa yale yakhusuyo Imani hiyo. Ni wajibu kukumbushana mara tunapoghafilika. In Sha Allah.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2016

    Haya tena hakuna jema!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2016

    Mdau wa pili hata hilo liilloelezwawa hapo juu ni jema kwa wenye imani yao. Yawezekana ikawa baya kwako, l jema kwa wenzako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...