Na Raymond Mushumbusi WHSUM.

Serikali imewapa miezi miwili wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani kilichopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam kuhama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na wananchi hao katika kikao cha kujadili na kukubaliana muda wa kuhama katika eneo hilo leo Jijini Dar es Salaam.

“Ndugu zangu tumejadiliana wote na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili mtakuwa mmeshaama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha michezo kwa ajili ya shughuli za mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw. Nkenyenge.Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa kuwahamisha wananchi hao unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo kitakachojengwa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali.

Kwa upande wake mmoja ya wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa amesema wamekubaliana na muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo kwa wenzao na kabla ya muda hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo hilo.Katika mpango wa kukuza na kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga kukuza sekta ya michezo nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali itakayochangia katika pato la taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akitoa agizo la kuhama kwa wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam(Hawapo Pichani) kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisistiza jambo mbele ya wajumbe wa kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya akichangia hoja katika kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Mafuku Rajabu akifafanua jambo katika kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.Eneo la Changamani kijiji cha Michezo ambalo wananchi wake wanatakiwa kuhama ndani ya miezi miwili kupisha uendelezwaji wa eneo hilo kwa ajili ya michezo mbalimbali.Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...