Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Ndanda umeweka wazi kuwa bado hawajapata ripoti ya kocha Abdul Mingange na wanahamu ya kutak kujua ni kipi ambacho wanatakiwa kukifanyia marekebisho hasa baada ya kumaliza Ligi wakiwa nafasi ya tisa na kujikusanyia pointi 35.

Afisa habari wa timu hiyo, Idrisa Bandari  amesema kuwa baada ya kumaliza salama msimu huu sasa wanasubiri ripoti ya mwalimu kuelekea msimu ujao kwani kwa sasa yupo katika maandalizi ya mwisho ya ripoti yake huku ikisubiriwa kwa hamu kuona nini amekipendekeza na msimu umemalizika kukiwa na changamoto nyingi na imani ni kwa mwalimu ili kuzifanyia marekebisho.

Amesema kuwa endapo kocha huyo atabainisha kila changamoto iliyowakuta kama timu basi msimu ujao wataingia ndani ya ligi wakiwa wazuri zaidi ya msimu huu. "Ligi ilikuwa na changamoto nyingi na kwa sasa tunachokisubiri ni ripoti ya mwalimu ambayo ipo katika maandalizi ili kujua ni sehemu zipi zinazohitaji marekebisho ndani ya timu", amesema Bandari.

Mapendekezo hayo yatakapofikishwa mezani watajua mchezaji yupi ataendelea kusalia ndani ya kikosi pamoja na wale watakaotenywa.

Akizungumzia suala la udhamini, bandari amesema kuwa uongozi wao umeshafanya jitihada kubwa za kutafuta udhamini ukiacha ule unaotolewa na wanaosimamia ligi hiyo.

"Kama timu tumeshafanya jitihada kubwa kuhakikisha tunapata udhamini mzuri ili tuweze kujiendesha vizuri na tunashukuru tupo katika hatua nzuri", amesema Bandari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...