Na. Frank Geofray – Jeshi la Polisi, Dodoma

Katika kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutamba nchini,  makamanda wa Polisi wa mikoa, wakuu wa upelelezi na waendesha mashtaka wameazimia kuboresha ushirikiano wao katika kufanikisha kesi za wahalifu pindi zinapofikishwa mahakamani ili waweze kupewa  adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamo katika maazimio ya watendaji hao wa haki jinai nchini katika kikao kazi cha siku mbili kilichofanyika  mkoani Dodoma na kuwashirikisha makamanda wa polisi wa mikoa,  mawakili wafawidhi wa mikoa  na wakuu wa upelelezi wa mikoa.

Kikao hicho kilikuwa chini ya uenyekiti wake Mkuu wa Jeshi la Polisi,  IGP Ernest Mangu pia kilihudhuliwa na mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DPP  Biswalo Mganga, Makamishina wa Polisi, pamoja na taasisi mbalimbali zinazohusika na upelelezi na uendeshaji wa mashtaka.

Wapelelezi hao na waendesha mashtka walisema wataendeleza  program za mafunzo ya pamoja katika ngazi ya mkoa, kufanya vikao vya mara kwa mara ili kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili  na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano lengo likiwa kuharakisha upelelezi  na kutoa haki kwa watuhumiwa.

Aidha,  wajumbe hao wa haki jinai wameazimia pia kukabiliana na changamoto ya ucheleweshaji wa upelelezi  wa kesi ambapo wamekubaliana kwa pamoja kuzifikisha mahakamani kesi zote zenye ushahidi wa moja kwa moja ili kuondokana na kesi kuchua muda mrefu na kuleta malalamiko kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...