Na:
Lilian Lundo – MAELEZO
Waimbaji
wa Nyimbo za Injili nchini wametakiwa kuifanya kazi hiyo kwa kujitolea ikiwa
kama sehemu ya ibada ya kumtumikia Mungu kwa kulitangaza neno lake na si
kugeuza kazi hiyo kuwa mtaji wa biashara.
Hayo yamesemwa na
Mwalimu wa kwaya ya Wateule Elikana Simatiya kutoka kanisa la Anglikani, St.
James lililoko Tabata Segera jiijini Dar es Salaam, maarufu kama kunyata
nyata jina lililotokana na nyimbo ya
kunyata nyata aliyoifundisha akiwa kwaya ya Mennonite.
“Waimbaji wengi wa
nyimbo za injili wameacha kutumikia Mungu na badala yake wamekuwa
wakiuunda vikundi binafsi vya uimbaji ambavyo hutumika kama vyanzo vya fedha na
hualikwa kwenye mikutano ya injili na sherehe mbalimbali kwa malipo maalum,”
alisema Simatiya.
Aidha ameeleza kuwa,
uimbaji wa nyimbo za injili ni wito kama ulivyo wito wa uchungaji lakini hivi
sasa muimbaji wa injili akialikwa katika mikutano ya injili au sherehe huomba
malipo hadi ya shilingi milioni moja.
Simatiya aliongeza
kuwa, ziko gharama ambazo muimbaji anaweza kuomba kupewa kama usafiri kwa ajili
ya kumfikisha eneo husika au malazi na chakula ikiwa atahitajika kulala nje ya
makazi yake, lakini waimbaji wa leo wamebadilisha wito wa kutangaza injili kwa
njia ya uimbaji kuwa biashara.
Hivyo mwalimu huyo
amewataka waimbaji kubadilika kwa kuacha kuharibu kazi ya Mungu na kufanya kazi
hiyo kwa kujitolea kwani wapo wanaopokea uponyaji na wanaotiwa moyo kupitia
nyimbo za injili.
Kwaya ya Wateule
inatarajia kuzindua albamu mpya ijulikanayo kama Wateule tutakwenda siku ya
Jumapili Mei 29, 2016 Tabata Segerea katika kanisa la St. James, ambapo mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda,huku
wakisindikizwa na waimbaji wa injili
ambao ni Ambwene Mwasongwe, Christina Shusho, Edson Mwasabwite pamoja na kwaya
za Anglikan kutoka Vingunguti na Ukonga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...