Na Eliphace Marwa MAELEZO

Jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi Ilala limewahakikishia usalama wananchi wa Mkoa wa kipolisi Ilala  na kuachana na taarifa za uvumi kuhusu hali ya usalama katika mkoa huo wa kipolisi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya  amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote na kutoa tahadhari kwa wahalifu kuwa makini kwani jeshi lake limejidhatiti ipasavyo.

“Niwahakishie wananchi kuwa hali ya ulinzi iko vizuri na jeshi la polisi Mkoa wa Ilala limejipanga vizuri hivyo wananchi wawe na amani kwani tunafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo wakati wote”, alisema Kamanda Mkondya.

Aidha kuhusiana na malalamiko ya wananchi wa Buguruni kuhusiana na kuwepo kwa kundi la vibaka na waporaji kamanda Mkondya amesema kuwa Jeshi lake linaendelea na operesheni ya kukamata wahalifu usiku na mchana ili kuhakikisha Mkoa wa kipolisi wa Ilala unakuwa salama ambapo mpaka sasa jeshi hilo linawashikilia baadhi ya wahalifu waliokuwa vinara wa uporaji eneo la Buguruni Chama.

“Mpaka sasa tunawashikilia vijana kadhaa ambao walikuwa ni kero katika eneo la Buguruni chama na maeneo mengine ya Mkoa wa Ilala”, aliongeza Kamanda Mkondya.

Kwa upande wake Afisa habari wa Manispaa ya Ilala Bw. David Langa amesema kuwa Manispaa yake kwa kushiriana na Jeshi la Polisi wako katika mkakati wa kuanza operesheni ya kuwaondoa wapiga debe ambao wamekuwa wakishtumiwa na wananchi kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala.

Aidha Kamanda Mkondya amewataka wakazi wa Ilala kutoa taarifa za kihalifu kwa jeshi lake ili kuweza  kuifanya Ilala kuwa salama na kutimiza dhana ya ulinzi shirikishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...