Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KAMATI ya watu wenye walemavu nchini (TPC) imeandaa fursa kwa kuanda mafunzo mbalimbali pamoja na  kutoa elimu ya michezo kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni lengo kuu  la kuondoa dhana kwa watu wengine na kuwajulisha kuwa ulemavu sio dhambi.

Akitoa rai hiyo pamoja na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa niaba ya Baraza la Michezo Taifa (BMT) Afisa habari Najaha Bakari amesema kuwa TPC wamepata fursa ya kuandaa semina hiyo elekezi baada ya chuo kikuu cha Kentucky cha nchini Uingereza wakiwa na lengo kuondoa fikra mbovu kwa watu wanaohisi kuwa walemavu hawana nafasi katika michezo.

"Kamati ya watu wenye ulemavu wamepata fursa kutoka kwenye chuo kikuu cha Kentucky na wamekuja kwa ajili ya kuandaa fursa hiyo itakayowalenga hususani walemavu mbalimbali na watakaa semina kwa siku tatu na mwisho kutakuwa na bonanza litakalohusisha michezo tofauti,"amesema Najaha. Michezo itakayokuwepo siku hiyo ni mchezo wa tennis, mpira wa wavu,mpira wa miguu na michezo mingine ambayo itawahusisha walemavu kiujumla.

Semina hiyo inaanza Mei 26-29 na itafanyika kwenye uwanja wa Taifa wa zamani huku Raisi wa TPC Gwakisa Mwakibete amewataka wazazi kuja kwa wingi pamona na vijana wao kuja kupata semina elekezi itakayokuwa na umuhimu sana kwao na kuwaondoa kwenye fikra potovu za kumuona mlemavh hawezi chochote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...