Kundi la Wasanii wa Hip Hop Weusi.
Na Mwandishi wetu Mtwara

Wasanii Aisha Ramadhani maarufu Isha Mashauzi na kundi la muziki wa Hip hop la Weusi wanatarajiwa kushiriki katika kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa malaria katika mradi unaojulikana kama KLINIKI CHANDARUA.

Mradi huo unaotarajiwa kutoa vyandarua bure kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa unazinduliwa jumamosi wiki hii Mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa matekelezo kutoka mradi wa Victor Works Bi, Noela Kisoka amesema wasanii hao watashiriki katika kuhamasisha kampeni hiyo kwa kupitia muziki na wao watashiriki katika uzinduzi wa mradi huo.
Isha Mashauzi

" Tunatarajia kuwa na wasanii kutoka katika kundi la Weusi ambao wanaimba muziki wa kizazi kipya lakini pia tutakuwa na mwanamuziki wa Taarab Isha Mashauzi ikiwa ni hatua ya kuufanya muziki kuwa sehemu ya hamasa ya utekelezaji wa mradi huu" alisema Kisoka.

" Wananchi wa Mtwara wajitokeze kwa wingi kutazama burudani ya muziki wa wasanii hao lakini pia kupata taarifa kuhusiana na Mradi wetu wa KLINIKI CHANDARUA ambao siku hiyo (leo) ndio tutauzindua" alisisitiza Kisoka.

Wasanii hao wamewasili jana jioni mkoani mtwara,tayari kuwasha moto katika uzinduzi wa mradi huo unaotarajiwa kufanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani hapa.

Mradi wa KLINIKI CHANDARUA utazinduliwa mkoani mtwara na mkuu wa mkoa huo Halima Dendego na unatekelezwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania, shirika la Victor Works na kudhaminiwa na shirika la misaada la marekani USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...