Kwa mara ya pili mwezi huu Uingereza imeondoka katika umoja wanchi za Ulaya, safari hii ikiwa katika michuano ya Euro 2016 baada ya vibonde Iceland kuwatandika bao 2-1 katika mzunguko wa mwisho wa michuano hiyo ya mabingwa wa Ulaya.
Mashabiki wa Uingereza walianza kwa shangwe na kuishia katika maumivu mjini Nice bada ya kupata bao la kuongoza dakika tatu tu za mchezo kabla ya kuachia dakika kumi baadaye. Kocha Roy Hodgson alijiuzuru mara baada ya mchezo kwa kukubali kuwa "hatoshi".
Alikuwa nahodha Wayne Rooney aliyeweka mpira kimiani kwa mkwaju wa penalty baada ya Raheem Sterling kuchezewa rafu ndani ya boxi, lakini Ragnar Sigurdsson wa Iceland akawasawazisha. Kisha Kolbeinn Sigthorsson akafunga la pili kwa mkwaju mkali uliomshinda kipa wa Uingereza Joe Hart.
Mashabiki wa Uingereza walionekana kutoridhishwa kabisa na timu yao iliyokuwa ikijitahidi kusawazisha ili kufika raundi ya pili kupambana na mtani wao wa jadi Ufaransa, lakini wapi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...