Na Dac Popos, Globu ya Jamii.
Fainali ya kibabe ilipigwa ndani ya dimba la Met Life Sport Complex, New Jersey nchini Marekani na kuishuhudia Chile ikitetea ubingwa wake kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Argentina. Kama ilivyokuwa mwaka 2015 Chile walishinda penati 4-1, safari hii imekuwa 4-2.

Mchezo ulianza kwa kasi huku Messi akiwasumbua mabeki wa Chile kitu kilichopelekea mlinzi Diaz kumchezea Messi rafu na kupewa kadi ya njano mnamo dakika ya 17, kama hiyo haitoshi dakika ya 28 Diaz kwa mara nyingine anamkwatua Messi na kupewa kadi ya pili ya njano ambayo inazaa kadi nyekundu.

Chile wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja wanajipanga vizuri na kuwa mudu Argentina, kunako dakika ya 42 mlinzi wa Argentina M. Rojo anamfanyia madhambi kiungo wa Chile Vidal na mwamuzi anamzawadia kadi nyekundu ya moja kwa moja na timu zote zinacheza na wachezaji 10.


Dakika 90 zinamalizika bila goli kwa timu zote, muda wa nyongeza wa dakika 30 nao unamalizika bila bao, hapo inafuata hatua ya MATUTA, ambapo Chile wapata 4 na Argentina wanapata 2. Waliofunga kwa upande wa Chile ni Castillo, Aranguiz, Beausejour na Silva huku aliye kosa ni Vidal ambaye penati yake iliokolewa na kipa wa Argentina.


Waliofunga kwa upande wa Argentina ni Mascherano na Aguero wakati waliokosa ni Messi aliyepaisha juu ya lango na Biglia ambaye penati yake iliokolewa na kipa.

Chile wanakuwa mabingwa wakati michuano hii inatimiza miaka 100 toka kuanzishwa kwake mwaka 1916.

Baada ya kauli ya Maradona kuwa Argentina wakishindwa kuchukua ubingwa wasirudi nyumbani je watarudi?......Pia inaonyesha kuwa Messi ni mchezaji mwenye mikosi na fainali kwani mwaka 2014 aliiongoza timu yake kucheza fainali ya kombe la dunia, wakapoteza dhidi ya Ujerumani.2015 wakapoteza fainali ya Copa Amerika dhidi ya Chile na mwaka huu 2016 wanapoteza tena kwa Chile, hilo ni gundu au?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...