Mwenye nguvu mpishe...

1. Simba ndiye paka mkubwa kuliko wanyama wote wa jamii ya paka na simba wa afrika wamekuwa maarufu kwa jinsi ya umoja, upendo na mshikamano wao na huishi kwa pamoja kwenye kundi la misifa na kundi moja la simba wanakadiriwa kuwa kati ya simba 10-40 wakiongozwa na mfalme wao.
2. Simba dume ndiye mlinzi wa kambi iluhali majike ndio wasakanyaji wa chakula (wawindaji) licha ya hayo, simba dume ndio wa kwanza kula na kwa wastani madume yanakula sana kuliko majike
3. Simba ni mmoja wa wanyama walio katika orodha ya hatari ya kutoweka kabisa duniani kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhifadhi IUCN

4. Simba wa kwanza walipatikana Afrika (sio Kenya), asia na Ulaya lakini yasemakana kwa sasa simba walio katika mazingira Afrika wanapatikana Afrika tu (sio Kenya) kweingineko wanaishia kuwaangalia simba kwenye mizingo yao wanyama (ZOO).
5. Ngurumo za simba zinafika/sikika umbali wa kilomita nane na daima atembeapo visigino vyake havigusi ardhi.

6. Simba wana uwezo wa kukimbia umbali wa maili  50 kwa saa na kuruka futi hadi 36.
7. Simba hulala masaa 20 kwa siku na hasa anapokua ameshiba. Simba huishi kwa wastani wa miaka 10-14 mwituni, huku katika hifadhi huweza hata kufika zaidi ya miaka 20.
8. Simba mkubwa hula mara moja tu kwa wiki wastani wa kilo 20-35 za nyama kwa mlo mmoja kutegemeana.
9. Ingawa simba hujulikana kama mfalme wa pori, simba wengi huishi kwenye nyasi tu na hupenda sana nyasi kavu na ndefu (ellephant grassland), hata rangi ya simba huakisi rangi ya nyasi kama mbinu ya mawindo ila ikumbukwe tu kwamba ubabe wa simba una wapinzani pia kama Tembo (ingawa meno ya mbwa hayaumani)
10. Simba dume anafikia urefu wa mwili pamoja na kichwa wa sentimita 170 hadi 250; kimo cha mbegani ni 120 cm. Dume mkubwa anaweza kuwa na uzito wa kilogramu 225. Jike ni mdogo wake akiwa na urefu wa 140 hadi 175 cm, kimo cha mbegani cha 100 cm na uzito wa 150 kg. Simba dume anatofautishwa kirahisi kutokana na manyoya marefu ya shingoni ilhali jike hana.

Ila yote hapo juu hayahusiani kabisa na 
Klabu ya Simba SC ya Tanzania tafadhali...

Compiled by Geofrey Chambua 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...