Juni 29,2016 kumefanyika tukio muhimu mjini Shinyanga ambapo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa (pichani) amewaandalia chakula cha pamoja “futari” waumini wa dini ya kiislamu mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuutukuza mwezi mtukufu wa Ramadhani. 
Tukio hilo limefanyika leo jioni/usiku kuanzia  katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na waumini na viongozi wa dini  wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya.
Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola akisisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali dini,makabila wala rangi zao.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu Makusanya akitoa shukrani za mualiko wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga kushiriki futari ya pamoja ambapo alisema hilo ni jambo jema linalofurahiwa sana na mwenyezi Mungu.
Viongozi wa madhehebu ya dini,serikali na dini ya kiislamu wakiwa meza kuu huku washiriki wengine wakiwa katika mstari kwa ajili ya chakula.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...