Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma 
 Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki harambee ya kuchangia waandishi wa habari kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya “Media Car Wash For Health” iliyofanyika leo katika viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma ambapo amechangia jumla ya shilingi milioni 5 ili kuokoa maisha ya waandishi wa habari. 
 “Kuna umuhimu mkubwa wa kuwachangia waandishi wa habari kwani wamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya nchi na kuhamasisha amani ya nchi, kwa kutambua umuhimu wao nitachangia shilingi 5,000,000 ili iweze kuwakatia Bima ya Afya,” alisema Mhe.Dkt. Tulia. Licha ya kuchangia fedha hizo Mhe. Tulia aliosha baadhi ya magari ya waheshimiwa wabunge kwa ajili ya kuchangia harambee hiyo ambapo kila mbunge aliyeoshewa gari yake alichangia shilingi 100,000 ambazo moja kwa moja ziliingia katika mfuko wa kuokoa maisha ya waandishi wa habari kwa kuwakatia Bima ya Afya. 
 Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendelea ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla amechangia shilingi 1,000,000/= ambayo nayo inaenda kusaidia waandishi wa habari ili waweze kukatiwa Bima ya Afya. 
 Lengo la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya afya zaidi ya waandishi wa habari 1000 hapa nchini. 
 Aidha harambee hii ni ya pili, harambee nyingine kama hii ilifanyika mwaka 2015, viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidia kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa wanaugua kwa kipindi kirefu.​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​
   Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki  harambee ya Media Car Wash for health mjini Dodoma leo. Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akiosha gari la Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota wakati wa kampeni ya Media Car Wash ya kuchangisha fedha za kusaidia wanahabari kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 


Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akizungumza na baadhi ya wabunge na wageni mbalim bali kuelezea lengo la kampeni hizo asubuhi njini Dodoma. 


Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani.
 
Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) wakishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ Dodoma leo.



Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun wakiosha moja ya magari yaliofika kuoshwa kwa ajili ya harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...