Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini  inapenda kuwafahamisha wananchi kwamba,  kuanzia tarehe 27 Juni, 2016 hadi tarehe 06 Julai, 2016 itaendesha zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992, kwa Vyama vya Siasa vyenye usajilli wa kudumu kwa upande wa Tanzania Bara.

Zoezi hili ni endelevu kwani  ni utekelezaji wa kawaida  wa majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.Hufanyika kila mwaka  isipokuwa kwa mwaka jana (2015) kwa kuwa  ulikuwa mwaka wa uchaguzi.
Zoezi la uhakiki kwa upande wa Zanzibar litafanyika baada ya zoezi kukamilika Tanzania Bara kwa tarehe ambazo zitatangazwa baadaye.

Ofisi inatoa rai kwa vyama vyote vyenye usajili wa kudumu kulipa kipaumbele zoezi hili, kwani ni zoezi ambalo linagusa uhai wa kila chama.



Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
24 JUNI, 2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...