Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 
 BAADA YA kupoteza michezo miwili sasa kikosi cha timu ya Yanga kinatarajiwa kuingia kambini Julai mosi kwa ajili ya maandalizi yao ya mechi zake za kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo kambi hiyo itakuwa nje ya Jiji la Dar es salaam huku wakiwa hawajaweka bayana ni wapi wataelekea. 
 Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry muro amesema kuwa wachezaji wamepewa siku mbili za mapumziko na Julai mosi kikosi kitaingia kambini. na tayari benchi la ufundi limeshakutana na uongozi na kuzungumzia mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi hiyo na baada ya kuona makosa yaliyojitokeza katika mchezo wao uliopita dhidi ya TP Mazembe sasa wanaelekeza nguvu katika mchezo wao huo ili kuhakikisha wanafanya vizuri. 
 Kwa sasa timu yao imebakiza mechi nne katika hatua hiyo hivyo maandalizi yatakayofanywa ni makubwa na watahakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao uliosalia dhidi ya Medeama pamoja na mechi za marudiano. 
"Kikosi kitaingia kambini kujiandaa na michezo yetu na tutahakikisha maandalizi yanayofanyika yanakuwa ya hali ya juu ili kuweza kupata pointi tatu katika kila mchezo", amesema Muro.
 Mechi inyofuata ya Yanga ni dhidi ya Medeama ya Ghana huku pia ikisubiri michezo yake ya marudiano na kufanya idadi ya michezo hiyo minne. 
 Licha ya mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuishangilia timu yao kwa nguvu zote lakini walishindwa kutumia nafasi walizozipata katika dakika 45 za kwanza na matokeo waliyoyapata ndo yameshatokea na hawawezi kubasilisha ukweli kuwa wamepoteza mchezo huo muhimu kwao tena katika uwanja wa nyumbani na zaidi uongozi wameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wao hivyo hawana sababu ya kumlaumu mtu kwa kupoteza mchezo huo. 
 Katika hatua nyingine Jerry alisema kuwa anataka wanayanga watambue kuwa madai ya wao kutakiwa kulipa deni la zaidi ya milioni 530 hazina ukweli wowote kama mchezo huo ulikuwa bure na hawakuingiza mapato yoyote, watatakiwaje kulipa deni hilo, 
"Kinachotuhusu sisi ni kulipia gharama za uwanja pamoja na vivu vingine muhimu hivyo kama kuna uharibifu wowote basi asilimia 15 ya fedha tunazolipa yatatumika kwa ajili ya uharibifu huo".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2016

    The mdudu, hiyo kambi hata muiweke juu ya anga ni sawa sawa na kutupa junia la Chumvi kwenye Bahari hivi ni viongozi gani hawa wasiojua tatizo la Yanga?Mbona sisi hata ambao sio viongozi tunajua kabisa tatizo la Yanga ni kutokua na miundo mbinu yake mwenyewe ambayo ni (1) kutokua na Academy ya kulelea vijana wenye talent ya football (2) kutokua na uwanja wake yenyewe haya ni maajabu ya Musa Club kama hiyo ya enzi na enzi kutokua na uwanja wake ndio maana mapovu yanakutokeni bila ya aibu eti team tunaipeleka Uingereza au sijui Uturuki ndio maana nimesema hata muipeleke mbinguni hamtopata matokeo chanya always mtabaki na matokeo hasi angalieni wezenu hao wanavyo kunyoweni nyie vichwa vya wendawazimu nendeni mkajunze kwa hao TP MAZEMBE muone walivyo jipanga kwa kila kitu na kwa taarifa yenu hawana hata wadosi kwenye team zao au hao wazee wenu mnaowaita WAZEE WA YANGA bado Simba na Yanga mko kwenye GIZA NENE

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2016

    Sheria na kanuni zinasemaje wakati viongozi wakiamua kupoteza mapato makusudi? serikali ya awamu ya tano inajitahidi kuongeza ukusanyaji wa mapato, sasa viongozi wameamua kupoteza zaidi ya TZS 95M ambazo serikali ingepata kupitia TRA kama VAT. Nini maamuzi ya serikali kuhusu hali hii? Na kama kila timu ikiachiwa kufanya hivyo itakuwaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...