Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu akila kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi. 
Muda mchache baada ya kiapo hicho mkuu huyo ameshiriki hafla fupi ya kukaribishwa na Chama Cha Mapinduzi katika ofisi za Chama hicho katikati ya mji wa Singida. Mhe. Mtaturu amesema kuwa ana dhamira ya dhati kuhakikisha wananchi wanapata maendelea shirikishwa hususani katika kuimarisha sekta ya elimu, afya, miundombinu na kukemea Rushwa ambayo inarudisha nyuma Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Mtaturu amesema kuwa ushirikiano baina ya serikali na wananchi wa Ikungi itakuwa turufu kubwa katika kuhakikisha wilaya inakomaa zaidi kimaendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...