Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani na Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya na Elimu kupitia program mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo nchini. Kutoka Kulia ni Makamu Mtendaji wa Rais wa Mfuko wa Abbott, Stephen Fussell na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund Bi.Elaine Leavenworth (katikati).
 Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) juu ya namna Mfuko wa Abbott ulivyojipanga kuendelea kutekeleza Program mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo za Matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika utoaji wa Tiba, maabara za kisasa, dawa na vifaa vya mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi.
Ujumbe  wa viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani ukimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake leo.
PICHA/ Aron Msigwa –MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...