Radio ya EFM imezindua jogging club na kushirikisha zaidi ya jogging club 30, jijini Dar es Salaam lengo kuu likiwa kujenga na kuimarisha afya. Uzinduzi huo uliopambwa na burudani mbalimbali ulikua wa aina yake ambapo, ulianza na jogging kuanzia makao makuu ya radio hiyo mpaka Mwenge na baadae kumalizikia Tanganyika Packers Kawe ambako tafrija fupi ya uzinduzi huo ilifanyika, hafla hiyo ilipambwa na mashindano ya mpira wa miguu na burudani ya muziki wenye asili ya singeli.

EFM Jogging Club imezinduliwa rasmi na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Mchechu ambaye ndiye aliyekua mgeni rasmi wa hafla hiyo ya uzinduzi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Efm Radio Denis Ssebo alisema kuwa, "lengo kuu la club hii ni kuimarisha afya pamoja na kusaidiana katika kujenga uchumi kwani tumeanzisha mfumo wa Saccos ambao utasaidia kukopeshana na kuwezeshana katika shughuli za kimaendeleo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu ambaye ndiye aliyekua mgeni rasmi akizungumza na wananchi (hapo pichani) kuhusu kuzindua wa EFM Jogging Club leo Julai 24,2016 katika viwanja Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Efm Radio Denis Ssebo akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo Julai 24, 2016 katika viwanja Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya asili ya singeli, Mc Makabila akiwapagawisha mashabiki wake kwenye uzinduzi huo leo Julai 24,2016 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
Sehum ya wananchi waliojitokeza kwenye zinduzi wa EFM Jogging Club leo Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...