Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Mabalozi wa Usalama Barabarani pamoja na Askari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara baada ya Naibu Waziri huyo na Mabalozi hao kuonyeshwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi hilo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka Mabalozi hao waendelee kushirikiana na Wizara yake katika kupambana na ajali nchini. Tukio hilo lilifanyika katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto (meza kuu), Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias AndengenyeNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Ilala, Ully Mbuluko jinsi chumba cha mawasiliano kinavyopokea miito mbalimbali ya matukio ya majanga. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiangalia Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakizima moto wakati tukio la moto linapotokea. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...