Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kupatikana kwa wachapishaji wa nyaraka bandia za serikali mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Augustino Tendwa.
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya cheti cha elimu ya juu ambacho kimepatikana toka kwa wachapishaji wa nyaraka bandia za Serikali mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya cheti cha ndoa ambacho kimepatikana toka kwa wachapishaji wa nyaraka bandia za Serikali mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (katikati) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya nyaraka bandia za serikali zilizopatikana toka kwa wachapishaji wa nyaraka bandia za Serikali mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa habari toka Idara ya Habari Bw. Frank Shija na kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Augustino Tendwa. Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo.

Serikali kuwachukulia hatua kali ikiwemo kutaifisha mitambo yao watu wote wanaojihusisha na uhalifu wa kughushi Nyaraka za Serikali na kuwataka  wananchi wasiowaamnifu wanaojihusisha na uhalifu wa kughushi na matumizi ya Nyaraka bandia waache mara moja.

Onyo hilo limetolewa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassian Chibogoyo katika Kipindi maalu cha “Tujikumbeshe” ambapo alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa kukamatwa kwa Nyaraka mbalimbali za Serikali leo jijini Dar es Salaam.

Chibogoyo amesema  mwaka 1999 Serikali ilitoa tamko kupitia Tangazo GN Na. 488 lililolenga kutahadharisha umma kuwa yeyote atakaye jihusisha na uchapaji wa Nyaraka bandia mitambo yake itataifishwa.

Serikali imekuwa ikiendesha Operesheni maalumu ijulikanayo “Okoa Pato la Taifa” ambayo lengo lake kuu ni kuhakikisha inapambana vilivyo na uharamia wa matumizi ya Nyaraka bandia.

Aliongeza kuwa uhalifu wa kutengeneza Nyaraka bandia ni zaidi ya ujambazi kwani zinaweza kuvuruga mipango ya nchi, na kusasabisha nchi kuingia katika hatari na machafuko.

Kwa mujibu wa Sheria za nchi matumizi ya Nyaraka bandi ni kwenda kinyume na sheria za nchi na adhabu zake zinafahamika. Akizitaja baadhi ya Sheria hizo Mpiga Chapa Mkuu amesema makosa ya uhalifu wa Nyaraka yanaangukia katika Sheria za Ushahidi,Sheria ya Makosa ya Jinai, Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1970 pamoja na Sheria ya Nembo na Alama za Taifa.

“Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1970 namba 3 ibara ya 6 inatoa katazo kwa mtu yeyote kumiliki Mihuri ya Serikali, Nembo ya Taifa na Karatasi maalum za Serikali kwa matumizi binafsi, mtu akikiuka sheria hii adhabu yake ni miaka 20 jela”. Alisema Chibogoyo.

Aidha ametumia fursa hiyo kwaomba wananchi wema kushirikiana na Serikali kupambana na vita hii kwa kutoa taarifa pindi wanapobaini waharifu wa namna hiyo kwani kuruhusu hali hii iendelee ni kuhujumu uchumi wa nchini.

Aliongeza kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamejipanga kuhakikisha wanashinda vita hii ili kunusuru uchumi wa Taifa nakuahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wasamaria wema watakao toa taarifa juu ya uhalifu huo.

Baadhi ya Nyaraka ambazo zimekuwa zikighushiwa mara kwa mara ni pamoja na Vyeti vya Elimu katika ngazi mbalimbali, Risiti za Serikali, Vyeti vya kuzaliwa na Ndoa, Stika za Bima, Kadi za Magari na Pikipiki, Mihuri na Nembo ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...