Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali  tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayokataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.

“Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.

Nakuongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.

Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).

Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.

Jaji Mutungi ametoa rai kwa  Viongozi wa Vyama vya Siasa  waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.

Katika tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa zitahusika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2016

    This is what loss of credibility engenders. Chadema is increasingly becoming a coalition of hooligans.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...