Mahali anapolala kijana Emanuel Fedrick (20)Mkazi wa Mwambeja Kata ya Ilemi jijini kwa zaidi ya Miaka 11 sasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuficha aibu ya familia. |
Kijana Emanuel Fedrick (20) mwenye tatizo la utindio wa ubongo akiwa amebebwa na shangazi yake Stella Mbuligwe baada ya kutoka nje na kufanyiwa usafi wa mwili. |
Mpendwa mhabarishaji wa habari HII, Kwanza napenda kutoa pongezi kwa majukumu yako ya kuhakikisha kwamba umma unapata habari mbali mbali ili kila mtu aweze kuchukua nafasi yake na kuifanya jamii yetu iwe mahali bora pa kuishi! Pili napenda kujitambulisha kwamba mimi ni miongoni mwa watu wanaoifahamu familia hiyo kwa takribani miaka minne sasa. Kwa hiyo napenda kutoa masikitiko yangu kwa mhabarishaji, kwamba taarifa hizi zimepotoshwa. Ninasema hivyo kwa sababu mimi nimemfahamu mtoto huyo kwa sababu amekuwa akitolewa nje na pia akishiriki chakula pamoja na wanafamilia wengine. Mimi mwenyewe ni shahidi, kwani nimewaona wazazi wake na wadogo zake wakimlisha. Si hivyo tu, bali wamekuwa wakimpeleka hospitali kwa matibabu; mimi mwenyewe nimeshawahi kufika katika hospitali ya Rufaa hapa Mbeya kumjulia hali mtoto huyu akiwa amelazwa. Kwa hiyo, tukio hili namna lilivyoripotiwa limeacha majeraha makubwa kwa wazazi na hata kwa mtoto mwenyewe. Napenda kutoa rai kwa wahabarishaji kufanya uchunguzi wa kina na kupata vyanzo sahihi, ili taarifa ziwe zenye kujenga badala ya kubomoa. Sio nia yangu kuanzisha malumbano katika hili, bali ninawaomba wahusika mfanye utafiti kabla ya kutoa habari. Waandishi ni kioo cha jamii, fanyeni hima kutupatia habari sahihi ili tuwe na mtizamo sahihi! Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki tasinia ya habari. Mungu iponye familia iliyojeruhiwa kutokana na upotoshwaji huu. Asanteni.
ReplyDelete