Picha na Habari na Frank
Mvungi-Dodoma
Naibu spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekabidhiwa ripoti ya uchaguzi
Mkuu wa Mwaka 2015 Bungeni mjini Dodoma leo.
Akizungumza
wakati akipokea Ripoti hiyo Naibu Spika amesema kuwa ripoti hiyo ni muhimu kwa
Bunge na ni kiashiria cha ushirikiano mzuri kati ya Bunge na Tume hiyo.
“Ushirikiano
uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mzuri na kwa upande wangu
natumaini tutaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali,” alisisitiza Mhe.
Dkt.Tulia.
Akizungumzia
majukumu ya Bunge naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia amesema kuwa Bunge la kumi na
moja limetimiza majukumu yake vyema hali
itakayochochea maendeleo hapa nchini
katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano
Kwa upande
wake mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva
amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tume hiyo na Bunge kama mdau muhimu
na kuahidi kuuendeleza kwa maslahi ya pande zote.
Ziara ya
Tume hiyo pamoja na kukabidhi ripoti hiyo kwa Naibu Spika ililenga kuwajengea
uwezo wajumbe wa Tume hiyo kuhusu majukumu ya Bunge ambapo wajumbe hao
walitembelea maeneo mbalimbali ya Bunge.
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imekabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ikiwa
ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva
akikabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Bungeni Mjini Dodoma mara baada ya Kuirishwa kwa Bunge jana.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu
Damian Lubuva na ujumbe wake wakiangalia moja ya vitabu vilivyopo kwenye maktaba ya Bunge
wakati wa Ziara yao Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi na Ujumbe wake mara baada ya ziara ya Tume hiyo Bungeni
Mjini Dodoma leo.kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva na kulia Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahamud Hamid.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu
Damian Lubuva akiongoza ujumbe wa tume hiyo kwenye viwanja vya Bunge leo wakati
wa Ziara ya kutembelea Bunge na kuwasilisha ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka
2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia
Ackson.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...