Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akimsikiliza Mjumbe wa Kikao hicho, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk. Zakaria Mganilwa (kulia) alipokuwa anachangia mawazo katika Kikao cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akimsikiliza Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (kulia meza kuu) alipokuwa akizungumza katika Kikao cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...