Baraza la taifa na Hifadhi ya Mzingira NEMC limepewa mwezi mmoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kupima Vumbi, Moshi na Maji yanayotoka katika kiwana cha kuchakata taka cha SBS kilichopo katika maeneo ya Mangamba Mjini Mtwara ili kujirisha kama vina madhara kwa maringira na viumbe hai.

Naibu Waziri Mpina akiwa katika muendelezo wa Ziara yake ya kukagua mazingira na kuangalia utekelezaji wa sheria ya mazingira kwa wenye viwanda nchini amelitaka baraza hilo kufanya kazi zake kwa umakini na kutokukubali majibu ya vipimo toka kwa mwenyekezaji bila NEMC pia kufanya vipimo na kupatamajibu sahihi kutokana na sababu kuwa wananchi wamekuwa wakilalamika mara kwa mara juu ya uchavuzi wa mazingira unaofanywa na wenye viwanda unavyo hatarisha maisha yao na mazingira kwa ujumla.

Katika Ziara Hiyo ya Mjini Mtwara, Naibu Waziri Mpina Pia alitembelea DAMPO la kisasa la mjini hapo lilijengwa kwa ufadhili wa Bank ya Dunia lenye thamani ya shilingi Bilioni 8.8 na kuwapongeza wana Mtwara kwa kupata Dampo la kisasa ambalo ni Rafiki wa Mazingira, na kuwashauri waratibu wa mradi huo na uongozi wa mkoa wa Mtwara kuanza kutumia DAMPO hilo ambapo taka zitakazowekwa katika DAMPO hilo la kisasa, pia zinaweza kutumika kutengeneza nishati mbadala.

Awali, akitoa taarifa ya Mazingira ya Mkoa wa Mtwara, katibu Tawala wa MKoa huo Bwana Afred Luanda, alisema kuwa Mkoa unakabiliana na changamoto mbali mbali za kimazingira ikiwa ni pamoja na uvuvi haramu wa kutumia mabomu, ukataji miti ovyo kwa matumizi ya kuni na mkaa, vifaa vya uondoshaji taka pamoja na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Ziara Ya naibu Waziri Mpina Mkoani Mtwara leo ilihusisha pia kutembelea bandari ya mtwara ili kujionea utekelezaji wa sheria ya mazingira katika uingizwaji wa viwatilifu na kemikali hatarishi kwa mazingira zinazoingizwa kupitia bandari hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (katikati) akikagua DAMPO mpya la kisasa la Mji wa Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira, katika ziara yake Mkoani humo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipata Maelezo kuhusu uchakataji wa taka unaofanywa na kiwanda cha SBS kutoka kwa Bw. Joseph meneja uendeshaji wa kiwanda hicho.

DAMPO la kisasa la Mjini Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira lililojengwa kwa hisani ya bank ya Dunia kwa thamni ya shilingi bilioni 8.8, mara DAMPO hilo litakapoanza kutumika litakuwa na uwezo wa kutengeza nishati mbadala. (Picha na Evelyn Mkokoi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...