Baada ya kuwadatisha washabiki katika maonyesho mawili makubwa kule bayreuth na tubingen sasa kamanda Ras Makunja anakipeleka kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni katika onyesho kubwa la XXL Afro Summer Jam mjini Stuttgart nchini ujerumani.
Onyesho hilo litafanyika siku ya jumamosi 30 Julai 2016 katika ukumbi mkubwa wa Kulturhaus Arena,uliopo Ulmer Str. 241, 70327 Stuttgart, Ujerumani.
Akiongea na vyombo vya habari kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja alisema Ngoma Africa band ni mali ya washabiki na ina kazi moja tu nayo kudatisha washabiki katika kila onyesho bila kurembaremba.
Bendi hiyo iliyojizolea umaarufu na maelfu ya washabiki kila kona duniani imejiwekea rekodi ya aina yake kuwa ni bendi ya mwanzo ya kiafrika kuimiri vishindo, na kudumu kwa miaka 23 ughaibuni na kufanikiwa kuwanasa washabiki wa kimataifa. ungana nao kupita Mtandao wao wa www.ngoma-africa.com au wape hi hapo www.facebook.com/ngomaafricaband
Kamanda Ras Makunja akiongoza mapambano.
Kikosi cha Mashambulizi kikifanya mabo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2016

    Kamanda na kikosi cha Ngoma Africa band pigeni kazini tunawategemeeni FFU wetu kila penye fujo lazima ukapatulize

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2016

    FFU wazee wa full gwanda Hapo Kazi tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2016

    FFU-Ughaibuni chini ya kamanda Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens hongereni sana kimataifa mnakubalika kazeni buti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...