Wanachama na mashabiki wa Yanga, usiku wa jana walikwenda nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara na kukabidhi mchango wao kwa ajili ya matibabu. Wanayanga hao waliongozwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro walimkabidhi Manara kiasi ya Sh 1,055,000 kama mchango wao. 

Wiki iliyopita, Manara aliamka na kujikuta jicho la kushoto halioni. Hivyo anatarajiwa kupelekwa India kwa ajili ya matibabu na safari yake huenda ikawa Jumamosi hii. 

Wanayanga hao walichanga fedha hizo kupitia makundi mbalimbali ya mitandao ya Wanayanga. “Nashukuru sana wenzangu, mchango huu mnaweza kuuona ni mdogo sana. Lakini ni mkubwa sana kwa kuwa gharama ni kubwa sana. “Nyie sasa mmredusha zile enzi za Yanga na Simba ambao walikuwa wakiishi undugu wa enzi zile. Msiba wa Yanga wanazika Simba na wa Simba wanazika Yanga. Hivyo ni jambo zuri sana,” alisema Manara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...