Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikabidhi leseni na funguo ya gari ya wagonjwa (ambulance) kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo (katikati) na anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naane (kulia). Gari hizo Nne aina ya Suzuki Maruti alizikabidhi katika  vijiji vya Masinono, Kurugee, Mugango na Nyakatende na kufikisha idadi ya gari Tano za wagonjwa alizozitoa katika Jimbo hilo.
Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kurugee wilayani humo, kabla ya kuwakabidhi gari ndogo ya wagonjwa aina ya Suzuku Maruti.
Wananchi wa Kijiji cha Kurugee wilayani Musoma wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) kabla ya kuwakabidhi gari ndogo ya wagonjwa aina ya Suzuku Maruti.
Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo (wa Pili kulia) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naane (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na na wananchi wa Kijiji cha Kurugee wilayani humo, mara baada ya kuwakabidhi gari ndogo ya wagonjwa iliyotolewa na Profesa Muhongo.

Wananchi katika Kijiji cha Masinono wilayani Musoma wakitazama gari dogo la Wagonjwa likiingia katika Zahanati ya Kijiji hicho. Gari hilo limetolewa na Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Gari hizo Nne aina ya Suzuki Maruti alizikabidhi katika  vijiji vya Masinono, Kurugee, Mugango na Nyakatende na kufikisha idadi ya gari  Tano za wagonjwa alizozitoa katika Jimbo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...