Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata akizungumza na waandishi habari juu zuio la taasisi za fedha na kampuni za simu kukata  miamala ya kodi ya ongezeko la thamani VAT leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kamishina wa Mapato ya Ndani wa TRA,  Elijah Mwandumbya.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishina Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata leo  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI  imezuia taasisi za  fedha  hasa benki pamoja na kampuni za simu za mkononi kutoza ongezeko la thamani (VAT ) kwa walaji (wananchi).

Akizungumza leo na waandishi habari  jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidata amesema kuwa fedha ambayo walikuwa wanakata haina ongezeko la thamani hivyo taasisi za fedha (Benki) kampuni za simu zimetakiwa zisiongeze miamala kwa wateja kwa kizingizio cha ongezeko la thamani.

Amesema kuwa fedha iliyokuwa ikikatwa imekuwa haikatwi hivyo kwa sheria hiyo inataka miamala  hiyo iliyokuwa ikikatwa ikatwe asilimia 18 ya thamani ya ongezeko.

Aidha amesema TRA haijaweka muongozo wa juu ongezeko hilo kwa taasisi fedha na kampuni za simu hivyo kwa watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua.

Kidata amesema kuwa wananchi wametakiwa wasiguswe kabisa katika ongezeko hilo kutokana na kutohusika na kufanya hivyo ni makosa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...