Salaam ankal na timu nzima ya Globu ya Jamii.

Mimi ni Mdau mkubwa sana wa Libeneka hili, na leo nimeona nilete kilio chetu kilio chetu dhidi ya Shirika la Tanesco ambapo naamini kuwa, wahusika wake pia ni wawasomaji wazuri wa libeneke lako hili. Sisi ni Wananchi wakazi wa Mwanagati - Kitunda Block 1 jijini Dar es Salaam na maeneo ya jirani tunatoa malalamiko yetu kwa shirika la TANESCO  kwa kutukatia umeme kwa siku tatu mfululizo usiku na mchana.

Tunaliomba shirika la TANESCO lisikilize kilio chetu haraka iwezekanavyo,na kuhakikisha tatizo la umeme linatatuliwa kwa wakati ili kutuepusha na adha tunayoipata hivi sasa sisi wakazi wa Mwanagati Block 1-Kitunda.

Mbali na matatizo hayo, Mji huo ambao ni mpya una chanzo chao cha kipekee na kikubwa cha maji kinachotegemea umeme katika uzalishaji wa maji na kutufanya kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yetu yazidi kuwa magumu zaidi.

Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la Tanesco ili kuelezea tatizo hili zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii, hivyo kupitia libeneke lako pendwa, tunaomba wasikie kilio chetu na kuja kututatulia tatizo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...