Wafanyakazi wa viwanda wilayani Mkuranga wamempongeza Mbunge wao Abdalla Ulega kwa kufanikisha kumleta Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama kwa lengo la kutembelea viwanda hivyo ili kujuwa kero wanazokutananazo huku akiagiza wanafanyakazi kupewa mikataba ya ajira zao.

 Waziri Jenista Mhagama ameagiza halmashauri ya wilaya ya Mkuranga kutengeneza sheria ndogo zitakazo kuwa zinasimamia masuala mazima ya kazi hususani viwandani na pia aliagiagiza viwanda hivyo kuhakikisha wanaweka awamu tatu za kuingia kazini ili kutoa fursa kwa wafanyakazi hao kufanya kazi kwa masaa nane kama sheria ya kazi inavyoelekeza kinyume na hapo lazima walipwe muda wa ziada kazini.

Jensta alitoa maagizo hayo leo wilayani hapa baada ya kufanya ziara ya kutembelea viwanda vya kuzalisha viatu na ndala aina ya yeboyebo huku akikemea vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa viwanda hivyo,ambapo ilidaiwa kuwa inafikia hatua ya kuwataka kimapenzi wanawake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akiwasili katika kiwanda cha ZFG kilichopo wilaya ya Mkuranga Kwa lengo la kusikiliza kero za wafanyakazi wa viwanda hivyo leo mkoani Pwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akizungumza na wafanyakazi wa viwanda vya kutengeneza viatu na ndala aina ya yeboyebo kuhusu kukemea vikali vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa viwanda hivyo leo mkoani Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wafanyakazi wa viwanda vya kutengeneza viatu na ndala aina ya yeboyebo katika ziara ya kutembelea viwanda hinyo mkoani Pwani, kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama.
Wafanyakazi hivyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama wakati alipofanya ziara mkoani Pwani. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...