Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijiniDar es salam Julai 28, 2016.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijini Dar es salaam Julai 28, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam baada ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijini Dar es slaam Julai 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kuondoa wafanyakazi wa mkataba kwa anjia ya kuwapa ajira ya kudumu kwa wenye sifa na kuwaondoa wasiokuwa na sifa ifikapo  Julai 30 mwaka huu. Amesema kitendo cha kutowaajiri na kuwatumikisha kwa mikataba kwa muda mrefu kinasababisha wakose stahiki zao jambo ambalo si halikubaliki.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Julai 28, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na kusisitiza kwamba ni lazima sula hilo lishughulikiwe haraka kwa sababu hayo ndio matundu watumishi hewa. “Mnawatumikisha watu kama vibarua kwa muda mrefu, hapa kuna wengine wanafanya kazi kwa mikataba kwa miaka mitano hadi sita hii haikubaliki kwani mnawakosesha stahili zao pale mnapowaachisha kazi,” amesema.

Awali Kaimu Ofisa Utumishi wa Manispaa hiyo Zaitun Hassan alisema wamekuwa wakitoa ajira za mikataba kwa sababu wamekosa watu wenye sifa za kuweza kuajiriwa husan madereva. “Kwa mara ya mwisho umetangaza lini nafasi za ajira? Katika mkoa wa Dar es Salaam kweli wanaweza kukosekana madereva wenye sifa za kuajiriwa? Alihoji Waziri Mkuu.

Zaitun alisema kuwa madereva wengi wanaojitokeza pindi wanapotangaza ajira wanashindwa kufikia vigezo ikiwemo kuwa na cheti cha VETA na badala yake wanakuwa na cheti cha kidato cha nne tu. Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa kuna wafanyakazi wengine katika Idara ya Uhasibu na Ujenzi ambao nao wameajiriwa kwa mkataba hivyo amemtaka Ofisa Utumishi kuomba kibali cha kuajiri kwa Katibu Mkuu Utumishi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufanya tathmini ya maeneo yote ya shule kwenye mkoa wake na watakaobainika kuingia katika maeneo hayo waondolewe haraka. Amesema baada ya kukamilisha utengenezaji wa madawati kinachofuatia sasa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambapo amezitaka halmashauri kuweka mipango  ya kujenga majengo ya madarasa ya ghorofa ili waweze kuwa na madarasa mengi katika eneo dogo.

Awali Waziri Mkuu alipokea msaada wa madawati 705 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Chamazi wilayani Temeke ambapo kati yake Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umetoa madawati 600 na Jumuia ya Mabohora imetoa madawati 105. Pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Agustino Mahiga alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 85 fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati.

Dk. Mahija alisema watumishi hao walichanga sh. milioni 100 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ambapo sh. milioni 15 wamekabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe ambaye alikuwa mtumishi wa wizara hiyo ili naye akatengeneze madawati kwa shule za wilayani kwake.


Kwa upande wake Balozi wa Kuwait nchini Jaseem Al Najem amesema Serikali ya Kuwait itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika shughuli zote za maendeleo hususan katika sekta za elimu na afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...