Kulia Meneja wa
Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) jinsi Mr Money wa Airtel Money atakavyogawa
faida ya shilingi billion
3 kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wake nchi nzima ikiwa ni faida
yao kutokana na kutumia Airtel Money kuanzia Januari hadi juni mwaka
huu kushoto ni Meneja wa uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando jana.
Kushoto
ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa kugawa gawio la faida ya
shilingi billion 3 kwa wateja
wa Airtel Money na mawakala wake nchi nzima ikiwa ni faida yao kutokana
na kutumia Airtel Money kuanzia Januari hadi juni mwaka huu. Kulia ni
Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa jana.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa gawio la faida la kila kiasi
cha shilingi billion 3 kwa wateja wake wa Airtel Money na mawakala
wakubwa na wadogo
nchi nzima
Airtel
imetoa gawio la faida kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi juni
mwaka huu ambapo kila mteja atalipwa sehemu ya faida kulingana na
kiasi cha salio lake katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku
Akiongea
na waandishi wa habari , Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando
alisema “Tunayofuraha kutoa gawio la faida la shilingi bilioni
3 kwa wateja wetu na wakala nchi nzima. Tunaamini gawio hili la faida
litawawezesha wateja wetu kutatua mahitaji yao ya kifedha na hivyo
kuthibitisha dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za kifedha”
“Tumejipanga
kuwawezesha wateja wetu kwa kupitia huduma na bidhaa tunazozitoa.
huduma ya Airtel Money imelenga kuleta unafuu na kuongeza upatikanaji
wa huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini hususani ya maeneo
ya pembezo mwa nchi. Aliongeza Mmbando
Mpaka sasa Airtel imeshatoa kiasi cha shilingi billion 10 kwa wateja na mawakala wa Airtel money tangu 2014.
Huduma
ya Airtel Money inawawezesha wateja kufanya miamala mbalimbali ikiwemo
kutuma na kupokea pesa, kulipia bili, kununua vifurushi, kuamisha pesa
na kutoa pesa
kutoka benki pamoja na kutoa mikopo isiyo na dhamana kupitia huduma ya
Airtel Timiza ambayo inatoa mikopo ya haraka, rahisi kwa wateja na
mawakala.
Mpaka
sasa mtandao wa mawakala 50,000 wa Airtel Money nchini Tanzania
wanaweza kutumia huduma hii. Theluthi moja ya mawakala wote wa Airtel
Money hutumia Timiza, na baadhi ya mawakala
sasa hivi wanakidhi vigezo vya kupata mikopo hadi Shilingi milioni
moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...