Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe
amezitaka asasi za kiraia zisiyumbishwe na misaada toka nje yenye mwelekeo wa
kukinzana na mila, desturi, utamaduni, imani za Watanzania, sheria na Katiba ya
nchi.
Mhe. Dkt Mwakyembe ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam
alipokutana na uongozi wa Taasisi ya Mtandao wa Jinsia Nchini (TGNP) ofisini
kwake na kuwaambia kuwa Serikali inaunga
mkono juhudi za asasi mbalimbali za kiraia kama vile TGNP za kuelimisha jamii na kutetea haki za watoto,
wazee, wanawake, walemavu na makundi mengine maalum yanayostahili fursa na
haki sawa katika jamii yetu lakini
haitazivumilia asasi ambazo zinaenda kinyume na maadili ya nchi na kukiuka sheria
na taratibu ambazo kama nchi imejiwekea.
“Serikali inaunga mkono kazi zinazofanywa na asasi za kiraia
nchini lakini niweke wazi kuwa
hatutazivumilia asasi za kiraia zinazoyumbishwa na misaada toka nje na
kujihusisha na vitendo ambavyo vinakiuka maadili, taratibu na sheria za nchi
ambazo zipo kwa mujibu wa sheria,” alisema Mhe. Waziri.
Alitolea mfano wa mashinikizo hayo kutoka kwa nchi zenye
nguvu kiuchumi duniani kama ya kutaka nchi zinazoendelea au asasi zikubali
ushoga na ndoa za jinsia moja kama sehemu ya haki za binadamu kama njia ya
kuendelea kupata misaada kutoka kwao na kuongeza kuwa asasi zenye muelekeo huo
nchini zinachunguzwa na zitakazobinika zitachukuliwa hatua kali.
"Nchi hizo zimekuwa zikitoa mashinikizo kwa nchi zetu
na hasa asasi nyingi zikizitaka zikubali ushoga na ndoa za jinsia moja,
tunazichunguza asasi zote za kiraia zenye mwelekeo huo na tukibaini mapungufu
hayo tutazichukulia hatua kali za kisheria, uchafu na upuuzi huo wa Wazungu,
ubaki hukohuko kwao," alisisitiza.
Waziri Mwakyembe alionya kuwa nchi ikilegeza kamba katika
suala hili, tutashinikizwa baadaye kufunga ndoa na wanyama wa kufugwa kwamba
nayo ni sehemu ya haki za binadamu.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Amon Mpanju,
alisisitiza umuhimu wa asasi za kiraia kuisaidia Serikali kwa kupeleka kwenye
jamii ujumbe sahihi wenye mafundisho badala ya kusubiri kukosoa tu na kuzitaka
asasi za kiraia kuacha kuunga kuunga mkono hoja za ushoga kwa kishawishi cha
fedha wanazopewa kutoka kwa wafadhili wao
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea katika kikao na watendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Katiba na S heria Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mtandao wa Kij insia Tanzania (TGNP) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju (wa tatu kulia) baada ya kumaliza kikao jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...