Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akitoa maelezo kuhusu mchango wa Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, Amir wa Kuwait katika masuala ya kibinadamu duniani.
Mhe. Dkt. Mahadhi J. Maalim, akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Waandaaji wa Vipindi vya Television kutoka Kuwait mara baada ya kumaliza mahojiano katika ofisi za Ubalozi Kuwait.

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, amefanya mahojiano na Wawakilishi wa Kituo cha Kurushia Matangazo ya Televisheni cha Kuwait (KTV) kuhusu mchango wa Kuwait katika masuala ya kibinadamu na maendeleo kwa ujumla.

Katika maelezo yake kwa Wawakilishi hao, Mhe. Dkt. Maalim, alisifu Juhudi za Amir wa Kuwait, Mtukufu Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, katika masuala ya kibinadamu na maendeleo kote duniani. Kufuatia mchango wake huo, Umoja wa Mataifa ulimpatia hadhi ya kuwa Kiongozi wa Misaada ya Kibinadamu pamoja na kuifanya Kuwait kuwa Kituo cha Misaada ya kibinadamu katika sherehe zilizofanyika Umoja wa Mataifa tarehe 9 Septemba 2014.

Aidha, Mhe. Dkt. Maalim, alipongeza kitendo cha Amir kuelekeza Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (KFAED) kutenga Dola za Marekani bilioni mbili kwa ajili ya kusaidia uwekezaji na maendeleo hususan ya miundombinu ya barabara kwa bara la Afrika wakati wa kilele cha Mkutano wa Viongozi wa Afrika na wa Kiarabu uliofanyika nchini Kuwait mwezi Novemba 2013.

Mwisho, Mhe. Balozi alimshukuru Sheikh Sabah pamoja na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zao zilizopelekea kufunguliwa kwa Ubalozi wa Kuwait, Dar es Salaam sanjari na ule wa Tanzania Kuwait hatua ambayo imewezesha kukua zaidi kwa mahusiano ya nchi mbili hizi. Vilevile, alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Kuwait katika kutekeleza miradi mbalimbali ya uwekezaji kwa maslahi ya pande zote mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...