Ankal Wasalaam,
 Wadau wote wa Blogu ya jamii, natumai mu wa wazima wa Kheri. Mimi mzima, na naendelea na kazi yangu ya u professor, nikifundisha masomo ya “Political Economics” hapa nchini Uingereza. Hii ni baada ya kumaliza Phd yangu pale Oxford University mwaka 2014 ambako nilikuwa Mwafrika wa kwanza kuvunja rekodi kwa kuandika thesis iliyokubalika na vyuo vikuu vikubwa duniani. Nadhani wasomi wengi wa hii blogu wananifahamu vizuri sana, kwa sababu bila mimi, hata John Mashaka asingeupata umaarufu alioupata. 
Niseme kwa kifupi nilimjenga John Mashaka, kwa kumsaidia sana kwenye utafiti kipindi akiwa chuo kikuu. Ingawa kila mtu ana kipaji chake cha kuzaliwa, ambayo nakiri kwamba Ndugu John anacho na ni Genius, ila pia lazima asaidiwe. Nimemsaidia mimi. Niko tayari zaidi kwenda kumsaidia Dr. Magufuli kujenga uchumi wa Tanzania.
Pamoja na wadau wengine, naungana nanyi kumuita John Mashaka atoke mafichoni na kurudi kwenye hii blogu ili mijadala ya kisomi iendelee. Nadhani Tanzania kama taifa hipo katika kipindi kigumu. Kipindo cha mpito ambapo mawazo chanya kama yangu, John Mashaka na genge lake wanaweza kuchangia. Nikiwa Professor anayeheshimika dunia nzima, kushirikiana na wakina Ndugu John Mashaka Hildebrand Shayo na wengineo kutawasaidia hata wao kukua zaidi na kujulikana kimataifa, licha ya kuleta mawazo chanya na mbadala katika ujenzi wa taifa letu.
Niko tayari kuendeleza mijadala ikiwa John Mashaka atajitokeza

Wenu katika Ujenzi Wa Taifa
Prof. US-Blogger, Bsc, Msc, PhD (Oxford)
Oxford University, Department of Economics
Political Economics
London, United Kingdom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. This is the most boastful fellow I have ever come across. US globber wewe ni kiatu na limbukeni mkubwa. So full of your self.

    ReplyDelete
  2. Heti niko tayari kwenda kumsaidia Rais Magufuli? Kijana ukitaka kuomba kazi, omba Kwa ustaarabu usitumie majina ya wengine. Hii ndio kawaida yako wasomi uchwata wa kuafrika. Heti Prof Dr. MSc. Bsc...hahahahaha. kazi kweli kweli. Job true true

    ReplyDelete
  3. Ankal
    Is this man real, or is this just a piece you wrote up to wind us up.
    If he is flesh and blood then he just forgot to add another degree to his list,,SDP...I will explain later.He is so full of himself, the way I read it he nearly claimed he created the other person.He thinks he can help the president to sort out Bongos problems by just a wave of his magical academic wand. Grow up.
    SDP stands for Self Deluded P..

    ReplyDelete
  4. Kwa kusoma hicho ulichokiandika ninama-shaka na u-professor wako. Kama ulimsaidia John Mashaka what is the big deal? Wewe leta hoja na si kujipiga kifua. Kama huko vizuri wewe peleka CV kwa JPM kwani longo longo za kupitia mlango wa uwani sasa hakuna

    ReplyDelete
  5. Huna jina ? weka jina lako ,,naona umejisifia sana mwenyewe ,,,weka jina tukujue ,,,Prof ,,Misifa

    ReplyDelete
  6. naomba mawasiliano yako ya simu Prof, pia Mr.John Mashaka naomba mawasiliano yako

    ReplyDelete
  7. Huyu US blogger ni mtu wa majigambo sana. Kama.kweli Ana uwezo wa kuchambua mada, nashauri ajikite mwenyewe kuliko kutumia mgongo wa John Mashaka, ili tujue mbivu na mbichi. Hizi ni tabia za kitanzania Heti Prof. Dr. Bsc. MSc, PhD. Sick fellow

    ReplyDelete
  8. Ankal, Huyu US blogger ni mgonjwa wa akili. Ila naona jina la John Mashaka ni dili watu wanataka walitumie kwenye hii blogu ili watoke nayo

    ReplyDelete
  9. SDP
    the P stands for prick, and look it up in crowdsourced dictionary not your fanciful Oxford Dictionary

    ReplyDelete
  10. Saa nyingine kichaa kaanzisha mjadala na sisi tunamjibu. Never argue with a fool No one will notice a difference. Alex bura dar.

    ReplyDelete
  11. Me nadhani nia ya huyu bwana mkubwa sio kujikweza bali ni kaamua kutumia fasihi vyema.so hii yote ni furahisha baraza tu na wala tusiichukulie u serious wowote bwna mkubwa huyu kaamua kutufurahisha tu

    ReplyDelete
  12. Ankal achana na hawa wazushi maprof. uchwara.

    ReplyDelete
  13. Ujinga tu, uprofessor gani ulionao wewe, WEKA JINA LAKO TUONE KAMA WEWE NI PROFESA MAARUFU...
    ANKAL nakushauri usi publish barua za wajinga kama hawa kwenye blog yako. chonde chonde

    ReplyDelete
  14. US Blogger, I can pity you saying that you assisted John Mashaka. The guy is in another leagues, and cannot comprehend you helping him, maybe it is the other way around. He helped you to copy and and paste your PhD thesis.

    You are full of yourself. You are reflect the majority of much know, with nothing to show for. Sad case study. You are nothing compared to John Mashaka for the blog readers who know both of you. By the way, are you a human being or an animal?

    ReplyDelete
  15. Ankal
    Can anyone explain to me why this man attracts such venomous attacks, that is above and beyond his obvious over inflated self-importance. He is a jerk but kama waswahili wasemavyo, pia ana damu ya kunguni

    ReplyDelete
  16. Nijuavyo mimi Oxford University iko Oxford sio London. Angalia anuwani yake Inanikumbusha shangazi yangu masikini aliyeniletea barua kwa anuwani yangu na kumalizia Glasgow, London, UK. Barua hiyo niliipata

    ReplyDelete
  17. Leave this US blogger alone. Going thru the 2014 Oxf.graduates, he is even not there.
    I think he is a "Hewa professor" ......look!!! Still he want to work with JPM.

    ReplyDelete
  18. JAMANI HUYU MTU KAWACHEMSHA TU..ALIKUWA AKIWAPIMA. .SASA ATAKUWA KAPATA JIBU LA WADAU WA MICHUZI WANAJAZBAH JUU KIASI GANI..THE GUY WASN'T EVEN SERIOUS. .KAMA HIVYO ANGETOA JINA LAKE.....CHECK KWANZA ALIVYOPANGA SENTENCE ZAKE..KWA UCHOKOZI...PUNGUZENI JAZBAH..KILA MTU ANAUHURU WA KUONGEA. .

    ReplyDelete
  19. Huyu jamaa alieleta hii article ni genius, alikuwa anafanya research kwa kupima vichwa vya wabongo, mpaka hapa kagundua kuwa vingi ni koroma, waliojibu juu wote wamejawa mapovu, hata jina hakuweka wewe unahamaki unaemkasirikia ni nani?

    ReplyDelete
  20. Mimi siamini kabisa kama kuna kitu kinachoitwa UHURU WA KUONGEA ama uhuru wa maoni yaani FREEDOM OF SPEECH, yaani total freedom ya mtu kusema chochote kile na wakati wowote ule, without restrictions without boundaries.Kama huniamini try this:
    Nenda Kariokoo na mwambie binti yeyote yule kuwa ameumbwa vibaya katika makalio yake,its free speech, lakini atakupiga kofi
    Nenda pale nje ya posta na upige kelele kama ungekuwa na bunduki ungewa....utakapopata fahamu tena, utajikuta una pingu na uko Ukonga
    So lets find another way of describing this freedom.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...