Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
TUME ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeaswa kuhakikisha tafiti zinazofanywa zijikite katika kutoa matokeo yatakayoweza kutatua matatizo ya wananchi na kuendelea kutengeneza ajira ili kuinua kipato cha wananchi na uchumi wetu kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako wakati wa kuzindua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Katika Kutekeleza agizo la Uchumi wa viwanda tunategemea rasilimali watu yenye ufahamu, ujuzi, teknolojia na ubunifu ili kuzalisha kwa tija na kuhimili ushindani wa kimataifa. 

Profesa Joyce amesema kuwa Tafiti zilenge katika kuimarisha uchumi wa viwanda zikiwa ni muhimu katika kuinua tija na uzalishaji, 
 “Baadhi ya tafiti za Kilimo zilizofanywa na taasisi zetu kama vile Chuo Kikuu cha Sokoine zimefanikiwa kutoa matokeo mazuri. Hii inajumuisha mbegu bora zinazoongeza mavuno kama vile mbegu za mihogo, mahindi na mpunga ambazo zinavumilia ukame na zinaweza kukinzana na magonjwa”. Amesema Profesa Joyce. 

Aidha amewaomba wakamilishe mapema taratibu zinazohitajika ili watanzania wengi waweze kunufaika na chanjo hizo muhimu kwa wafugaji wa kuku.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Hassan Mshinda amesema kuwa tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeweza kupata  chanjo inayozuia magonjwa ya kuku kama vile mdondo, ndui na mafua katika chuo Kikuu cha Sokoine.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa sayansi wakati wa kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Hassan Mshinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu  jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya wanasayansi wakiwa katika kongamano la wanasayansi jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako  akipata maelekezo juu ya kifaa kinachopiga picha za Juuu(Drone) jijini Dar es Salaam leo mara baada kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...