Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara, Bibi. Janeth Mayanja akiwa ofisini kwake.

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO.
MKURUGENZI Mtendaji  wa Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara, Bibi. Janeth Mayanja amemsimamisha kazi mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji kwa kosa la kujipatia fedha kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

Akizungumza leo mjini Bunda wakati wa tukio hilo, Bibi. Mayanja alisema kuwa ameamua kumsimamisha kazi  kwa muda, Bw.Eliudi Haonga ambaye ni mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji pia ni Mthamini wa Halmashauri  hiyo ili kupisha uchunguzi  kwa kosa la kujipatia fedha kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

“Tarehe 28 mwezi Juni mwaka huu  Bw.Eliudi Haonga alipokea  fedha kiasi cha shilingi milioni saba kutoka  kiwanda cha Olam ikiwa ni kodi ya pango kwa mwaka kodi 2015/2016, lakini mtumishi huyo  alihifadhi kwenye akaunti ya Halmashauri ya mji yaani ‘own source’ fedha kiasi cha  shilingi milioni mbili tu, na kiasi kilichobaki yaani milioni tano  alizitumia kwa masuala binafsi kinyume na taratibu za utumishi wa umma” alisema Bibi  Mayanja

Aliongeza kuwa Bw. Haonga aligushi risiti ya Halmashauri ya Mji na ambayo aliikabidhi katika  kiwanda cha Olam baada ya kupokea fedha hizo.

Alisisitiza kuwa mtumishi huyo amesimamishwa kazi kwa mujibu wa kifungu namba 38 (1) cha kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003.

Aidha, Bibi Mayanja  amewaasa watumishi wa umma wanaofanyakazi katika Halmashauri hiyo  kuwa  waadilifu kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi. Vile vile ameonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. DED naye ana maswali ya kujibu.
    1. Mtumishi ambaye sii mhasibu anapokeaje fedha?
    2. Taaluma ya mtumishi ni afisa ardhi... wapi na wapi kupokea fedha za pango?
    kwa kweli hela ya umma inaliwa hovyo hovyo.. JPM kaza buti kinoma

    ReplyDelete
  2. SAFIIIIIIIII.HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...