August
9 ya kila mwaka, dunia huadhimisha Siku ya Usomaji Vitabu Kwa kila
rika (International Book Lovers Day). Katika kusheherekea siku hiyo hapa
nchini, Taasisi ya Doris Mollel chini ya Mwanzilishi wake, Bi. Dorice
Mollel ilipata wasaa wa kutoa
vitabu kwa shule tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Shule za
Sekondari za
Tegeta na Mtakuja, pamoja na shule ya msingi ya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere. Vitabu hivyo vilitolewa kwa ufadhili wa Rehema Trust Foundation
kwenda kwa Doris Mollel Foundation.
Tegeta Sekondari ilipata vitabu ishirini na mbili (22), Mtakuja Sekondari ilipata
vitabu kumi na tisa (19) na shule ya msingi ya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ilipatiwa vitabu nane (8), pamoja na kuwashirikisha wanafunzi hao kati michezo iliyotolewa kwa
ufadhili wa Turkish Airways ili kusaidia watoto wapende michezo na
kuchangamsha ufahamu wao.
Mwakilishi
wa Taasisi ya Doris Mollel, Edward Allan akizungumza na wanafunzi wa
shule ya Sekondari Tegeta kuhusu umuhimu ya kusoma vitabu vya kiada,
mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo.
Mwakilishi
wa Taasisi ya Doris Mollel, Edward Allan akiwaonyesha kitu wanafunzi wa
shule ya Sekondari Tegeta kwenye moja ya vitabu vilivyotolewa kwao.
Mwakilishi
wa Taasisi ya Doris Mollel, Jerome Calvin (kulia) akimkabidhi vitabu
Mmoja wa Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakuja.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwalimu J.k Nyerere wakicheza na kufurahia mchezo wa chase uliotolewa na Taasisi ya Doris Mollel.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...