Na TFF
Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA), kwa mara nyingine limeipa nafasi Tanzania kwa kutoa kozi
maalumu ya stamina (Physical fitness) kwa makocha wa Tanzania wenye leseni
kiwango B inayoanza leo Agosti 22, 2016. Kozi hiyo inayoendeshwa na mkufunzi
kutoka FIFA, Dk. Praddit Dutta, raia wa India itafikia ukomo Ijumaa wiki hii.
Akifungua
kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliishukuru FIFA kwa namna
inavyoipa nafasi Tanzania katika kozi mbalimbali hususani za ukocha na uamuzi.
“Si kila nchi inapata privilege
(fursa) kama hii. Bila shaka FIFA inatambua uwezo wa makocha wa Tanzania kwa
sasa. Mjue kuwa FIFA ina watu wa kuwapa taarifa kila kona. Kama mngekuwa
mnafanya vibaya, FIFA wangesema Tanzania bado, kwa hiyo kozi zisipelekwe… lakini
inaonekana mnafanya vema, mngefanya vibaya msingefikiriwa,” alisema Mwesigwa
aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo.
Mwesigwa amesema kwa kuwa FIFA ina
malengo chanya na Tanzania kwa kutoa kozi mbalimbali ikiwamo hiyo ya physical
fitness inayolenga kuwapa ujuzi makocha hao kuwajengea uwezo wachezaji kuwa na
stamina.
Hivyo akawataka makocha
wanaohudhuria kozi hiyo kutumia fursa hiyo ya mafunzo si kwa ajili yao peke yao
bali kuendeleza ujuzi huo kwa wengine ambao hawakubahatika kuwa sehemu ya
wateule wa FIFA.
Naye, Mkufunzi wa kozi hiyo, Dk.
Dutta alisema: “Bila shaka Tanzania inakwenda kufungua ukurasa mwingine wa soka
la weledi kwa kuwa na wataalamu mbalimbali katika ukocha na uamuzi.
Mnachotakiwa ni kujitahidi kufanya vema na kozi nyingine nyingi zinakuja.”
FIFA kwa kushirikiana na Idara ya
Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mkurugenzi
Salum Madadi, imepitisha majina ya makocha 27 kuhudhuria kozi hiyo inayofanyika
katika Hosteli ya TFF iliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala
jijini Dar es Salaam.
Makocha wanashiriki kozi hiyo ni
Mohammed Muza, Samwel Moja, Nassa Mohammed, Jemedari Said, Oscar Mirambo, Wane
Mkisi, Cletus Mutauyawa, Shaweji Nawanda, Kizito Mbano, Dennis Kitambi,
Sebastian Nkoma, Fikiri Mahiza, Nyamtimba Muga, Nassor Mwinchui, Alfred Itaeli,
Henry Ngondo, John Tamba, Kidao Wilfred, Luhaga Makunja, Mohammed Tajdin,
Mohammed Silima, Salum Ali Haji, James Joseph, Kessy Mziray, Daudi Sichinga,
Bakari Shime na Salum Mayanga.
|
Home
Unlabelled
FIFA YAONGEZEA UJUZI MAKOCHA TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...