Ankal akiwa na keki yake aliyozawadiwa na familia yake katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo. Anamshukuru Mola kwa kumwezesha kufikisha siku hii adhimu na anaendelea kumuomba amjalie afya njema na baraka tele. Pia anaishukuru familia yake, ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wafanyakazi wenzake pamoja na makamanda wa tasnia ya habari kwa salamu za heri walizomtumia.
Wote anawaambia amezipokea salamu hizo kwa kuguswa moyoni na kuwaahidi kuendelea kuwa "mtoto mzuri" na kuendeleza libeneke la Globu ya Jamii ambayo mwezi Ujao Septemba 8 itatimiza miaka 11.
Keki imetengenezwa SWEET HANDS DELIGHT  ya Kawe karibu na Kanisa Katoliki. Namba zao 0713 925071/0714 590165

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. KEKI HAITENGENEZWI, BALI HUWA INAOKWA! KEKI IMEOKWA.......
    Dr Bitozi.

    ReplyDelete
  2. Ankali tunakutakia kila la heri,afya bora na maisha marefu, ombi letu tunaomba FULANAZZZZ ya blogu ya jamii irudi uliongoni
    wadau FFU-ughaibuni

    ReplyDelete
  3. KILA LA HERI,LAKINI MIAKA MINGAPI VILE??

    ReplyDelete
  4. Miaka mingapi Ankal au ni siri? Hongera

    ReplyDelete
  5. Hii kamera hapo juu nayo ni ubunifu wa mpiga keki au imepambwa tu.

    ReplyDelete
  6. Amefikisha miaka mingled?

    ReplyDelete
  7. Ankal ana miaka 47 sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...