Imekusanywa na Geofrey Chambua

Yasemekana mapacha ni watu ambao hupendwa sana na jamii kwa muonekano wao pia.

Ufuatao ni ukweli wa kushangaza kuhusu watoto mapacha.

1. Yumkini Mapacha wanaweza kuzaliwa na Baba wawili tofauti iwapo mama atajamiiana na wanaume wawili tofauti akiwa kwenye kipindi cha kushika ujauzito (ovulation period) ......ingawa wanasayansi wanasema uwezekano ni mtoto 1 kati ya watoto 400

2. Uwezekano wa kuzaa watoto mapacha umeongezeka sana hadi kufikia 76% tangu 1980 hadi sasa na hasa kutokana na ukweli kwamba wanawake wengi kwa miaka ya karibuni wamekuwa wakishika ujauzito haliyakuwa umri umesogea na wengi wana uwezekano wa kupata mapacha iwapo watazaa katika umri wa miaka 30 na kuendelea (wanawake katika umri wa 30yrs wana uwezekano mkubwa kuzaa mapacha kuliko wanaume katika umri wa 20yrs).....sababu za wanawake zinaelezwa ni kutokana na kuzalisha homoni nyingi za 'kiraghbishi' katika umri huu na hasa wanaposhika ujauzito katika umri wa miaka 35 (Follicle Stimulating Hormones). 
3. Utafiti uliofanywa na Taasisi moja ya Lafudhi ( Institute of General Linguistics) umeonesha kwamba watoto mapacha hujifunza matamshi baina yao wenyewe kwa njia ya kubwabwaja (babbling) na zaidi ya 40% huunda lugha tashtiti kwa mawasiliano baina yao (privacy) wakingali wadogo (cryptophasia)

4. Mapacha wengi huakisi taswira kinzani baina yao wenyewe wiki 14 tu baada ya ujauzito, mathalani pacha mmoja anaweza kuwa na alama fulani ya kuzaiwa upande wa kushoto ilihali mwingine ikawa upande wa kulia ama mmoja akawa mashoto na mwingine akawa malia japo mashoto wana weledi mkubwa sana wa kufaragua kuliko malia. Utafiti unaonesha kwamba baada ya wiki 28 mapacha huanza hata kushikanashikana (sio ngumi) wangali tumboni.

5. Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah kati ya mwaka ya 1800 hadi 1970 umeonesha kwamba watoto mapacha hurefusha maisha ya mama zao, yaani mama mwenye watoto mapacha ana uwezekano wa kuishi miaka mingi sana kuliko asiye na mapacha

6. Mapacha huanza kufumbatana na kufungama wiki 14 tu baada ya mimba kutungwa. Mwaka 2008 wanandoa maharimu huko Uingereza, walijigundua kwamba walizaliwa mapacha kwani mara tu baada ya kuzaliwa walitenganishwa na kwenda kulelewa na wazazi tofauti (adopted) kabla ya kuona wenyewe kwa wenyewe, dhahiri shari ilibidi ndoa ya ibatilishwe (annulled) na mahakama.
7. Unadhani mapacha wawili wa kiume (identical male twins) wakioa mapacha wawili wa kike (identical female twins), watoto wao watakuaje kisheria?.....Hao ni ndugu wa damu

8. Mama ambaye amewahi kuwa na jumla ya watoto 69 kwa uzao wa tumbo lake, akiwa na umi wa miaka 40 tu tayari alikua na mapacha 16!!!. Mama huyu amefariki mwaka 2010 akiwa na miaka 93!!!

9. Kila mtu duniani ana kinasaba chake (DNA) ingawa ni tofauti kwa mapacha wa kulandana (Identical twins) kwani DNA ziko sawa bin sawia . Hata hivyo hutofautiana alama za vidole (finger print) ambazo ingawa hulandana wakati wakiwa kwenye kijusi (embryos) , alama hizo huachana baada tu ya kijusi kutengana

10. Jimbo la Massachusetts nchini Marekani ndilo linaloongoza kwa kuwa na mapacha wengi duniani, idadi ya mapacha huko ni 20% ilihali Nigeria ikiongoza kwa mapacha wa kulandana (ingawa Nigeria inaongoza kwa mengi pia ikiwamo 'usanii')

11. Uwezekano wa wanaume mapacha kuzaa watoto mapacha utategemea na uwezo wa mwanamke ikiwa anaweza kuzalisha mayai mawili kwa mkupuo

12. 22% ya Mapacha ni mashoto ukilinganisha na 10% ya wasio mapacha duniani, ipo nadharia 'mizania' kwamba mazoea haya huanzia tumboni kutegemea na ......
13 Hii nimeipenda ya Viongozi wakuu wa nchi waliokua mapacha nchini Poland, Marehemu Lech Kaczynski (1949-2010) alikua pacha wa kulandana na Jaroslaw Kaczynski na wote wakichapa siasa. Wakati Lech alikua Rais wa Poland tangu 2005 hadi 2010, Jaroslaw yeye alikua Wazii Mkuu wa Poland kutoka mwaka 2006 hadi 2007. 

Yasemekana George W. Bush ndiye amewahi kuwa Raisi pekee duniani kuwa na mapacha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. katika nchi za Dunia ya kwanza, Kumekuwepo na mfumko mkubwa wa dawa zinazowawezesha wanawake wazae mapacha, wanawake wa nchi zilizoendelea huchagua kuzaa mapacha wawili, watatu hata wanne kwa kutumia dawa zinazopatikana kiurahisi,vile vile kumekuwepo kwa elimu inayowazeshesha kuchagua kuzaa mtoto wa kike au wa kiume, wakati mapacha wanaopatikana kwenye bara la Africa wengi ni DNA za asili tofauti na wa nchi zilizoendelea
    wanawake wa nchi hizo wamekua wakitumia muda wao mwingi wa ujana kusoma na kufanya kazi na kujiweka katika maisha ya hali ya juu, pindi wanapofikia umri mkubwa huamua kwenda hospitali kupatiwa dawa za kuzaa mapacha ili wasipoteze miaka mingi kubeba mimba kwani muda kwao ni pesa

    ReplyDelete
  2. ASANTE SANA umeniongezea kitu ambacho ninadhani kina mantiki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...