Katika kupunguza kasi ya uhalifu na kuwawezesha Vijana wa Iringa, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alikutana na vijana wa kijiwe cha Kihesa, ambao wengi wao wanajishughulisha na kuosha magari na kuwaomba kusaidiana naye katika kutokomeza udokozi.

Vijana hao walimuomba Mkuu wa Wilaya awasaidie upatikanaji wa mashine ya kuoshea magari ambayo aliwahidi kuwatafutia ndani ya siku 2 ili mradi wajiunge kwenye kikundi na wafungue akaunti benki. Vijana hao walimsukuru sana mkuu wa wilaya na kuahidi kuwa watiifu wa sheria na kuchapa kazi. Kikundi hicho kina vijana 25.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifanya mazungumzo na Kikundi cha vijana 25 wanaojishughulisha na uoshaji wa magari katika eneo la Kihesa, Mjini Iringa.
Kasesela akipitia taarifa ya Kikundi hicho aliyokabidhiwa.
Akitoka eneo hilo baada ya kumaliza kuzungumza na vijana hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Vijana walio vijiweni wawezeshwe kuona fursa zilizopo katika sekta mbali mbali ikiwemo ujenzi, kilimo, ujasiriamali, ili wasikae bure na kupoteza muda. Wengi wanahitaji kuhamasishwa na kuelezwa jinsi ya kujishughulisha katika mazingira waliyonayo na pengine mtaji mdogo ili wajitegemee.

    ReplyDelete
  2. Umeongea vizuri sana mdau wa kwanza lakini kwa bahati mbaya si viongozi wala wahamasishaji wenye kuliona hilo, si ajabu ikawa ni mtaji kipindi cha uchaguzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...