Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ametoa wito kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili waache kazi hiyo baadala yake watafute kazi nyingine zitakazoweza kuwaingizia vipato halali kwa kufanya hivyo wataweza kujiepusha kutiwa nguvuni na askari wanyamapori waliobobea kwa kazi hiyo. 
Maj. Gen Milanzi alitoa wito huo jana wakati wa akifunga mafunzo maalumu ya kupambana na Ujangili kwa askari wanyamapori katika pori la akiba la Rungwa mkoani Singida yaliyofadhiliwa na Marekani na yaliyotolewa na Kikosi maalum cha wanajeshi kutoka Marekani. 
 Amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa askari wanyamapori ili kuendelea na kukabiliana na wimbi kubwa la ujangili kwa kuwa majangili wasasa wanatumia silaha za kisasa tofauti na majangili wa zamani ambao walikuwa wakitumia upinde na mishale. 
 Aliongeza kuwa majangili wa sasa ambao askari wanyamapori wamekuwa wakikabiliana nao maporini ni wale ambao wanatumia silaha za kivita hiyo ni lazima askari wetu wapewe mafunzo ya hali ya juu ili waweze kukabiliana nao. 
Aidha Katibu Mkuu, Milanzi alisema Wizara imejipanga kuhakikisha suala la ujangili linakwisha ambapo kituo kingine cha mafunzo ya kijeshi kwa askari wanyamapori cha Mlele kilichopo Mkoani Katavi kimeanzishwa mbali na vyuo vya Pasiansi na Mweka, Likuyu Sekamaganga ambavyo pekee ndivyo vilivyokuwa vikitoa mafunzo kwa askari wanyamapori. 
 Aliongeza kuwa, kwa sasa Serikali imejipanga kwa kushirikiana na Interpol kuhakikisha kuwa hatakamatwa jangili tu aliyehusika kuua mnyama porini bali mtandao wote utakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria mahali popote. 
 Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo, Milanzi alisema mafunzo hayo yamejikita kuwasaidia kupambana na majangili, magaidi pamoja na majambazi ambapo wao ndo watu wa kwanza kukumbana nao wakiwa porini kwani ndiko wanakotumia kujificha kwahiyo ujuzi walioupata umewaongezea ufanisi katika kulinda maliasili zilizopo kwenye maeneo yao. 
 Aliwataka pia wahitimu hao kufanya kazi kwa kujituma wasiishie tu kusherekea kumaliza mafunzo bali waonyeshe kwa vitendo hii itasaidia na kuipa ari Marekani pamoja na Asasi za kimataifa zenye lengo la kusaidia nchi katika vita dhidi ya Ujangili. 
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress amewataka wahitimu wazingatie mafunzo waliyopata kwa kuyafanyia kazi ili Pori la Akiba la Rungwa liwe sehemu salama kwa wanyamapori wanaopatikana katika pori hilo.
 Ameahidi kuwa nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania kwa kuwa suala la ujangili bado ni kubwa linalohitaji ushirikiano wa pande zote ili liweze kutokomezwa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akifunga mafunzo maalum ya kupambana  na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na  majangili.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania
 ( TAWA) akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya ya kupambana  na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na  majangili. 
Askari wanyamapori wakionesha kwa vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu  yaliyofanyika katika Pori la Akiba la Rungwa  Mkoani Singida 
Askari wanyamapori wakionesha kwa vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu  yaliyofanyika katika Pori la Akiba la Rungwa  Mkoani Singida 
Askari wanyamapori wakionesha kwa vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu  yaliyofanyika katika Pori la Akiba la Rungwa  Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna ya kupambana na majangili  wakati  wakimkama ta jangili akiwa amejisalimisha yeye mwenyewe. 
 Picha zote na Lusungu Helela- MNRT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...